Mnamo mwaka wa Elfu mbili na tatu (2003), Rais mstaafu,Mwai Kibaki,
alizindua mpango wa masomo ya bure katika shule za msingi za umma.
Lakini je,
wafahamu kuwa hata baada ya sera hiyo ya serikali, hali katika kaunti ya Garissa,
Wajir na Mandera ni tofauti kabisa, kwani katika baadhi ya shule, wazazi ndio
hugharimika katika masomo ya watoto wao, ikiwamo mishahara ya walimu; huku
walimu walioajiriwa na serikali, wakilipwa mara moja kwa mwaka. Shadrack mitty
amerejea kutoka maeneo hayo na hii hapa taarifa yake.