Wednesday, August 27, 2014

GARISSA WOMEN REPRESENTATIVE, HON. SHUKRAN CLAIMS "ABUSE" BY BEING CALLED "SUPER"

I don't know what the Guys at Madogo Bridge, Tana River County want from our "own" Garissa County Women Representative, Honourable Shukran Gure by calling her Honourable "Msupuu"...Can you give her respect please....

Read Here.............or Continue Reading..


WABUNGE Katika bunge la Kitaifa, Kenya Jumanne waliangua kicheko pale Mwakilishi wa Wanawake, Kaunti ya Garissa Bi Shukran Gure alipodai kuwa maafisa wa usalama katika kizuizi cha barabarani cha Madogo, Tana River walimdhulumu kwa kumwita, "Msupuu".
Akitoa taarifa ya kibinafsi  bungeni kulingana na Sheria za Bunge nambari 84, Bi Gure alitaja matamshi ya maafisa hao wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) kama yaliyomdhalilisha "ilhali mimi ni Mheshimiwa aliyechaguliwa na watu wa Kaunti ya Garissa". 

Mheshima Spika kando na kuita majina kama vile ‘mrembo’ ‘msupuu’ maafisa hao wa jeshi ambao hukagua magari katika kizuizi cha Madogo walimhangaisha dereva na mlinzi wangu licha ya wao kujitambulisha kwao," akasema Bi Gure huku wabunge, hasa wanaume wakiangua kicheko kwa sauti za juu. Mbunge huyo aliwataka maafisa wa usalama kuwaheshimu wabunge, hasa wale wa kike. 

Hata hivyo wabunge wanawake wakiongozwa na Wabunge Ceciliy Mbarire (Runyenjes) na Florence Kajuju (Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Meru) walionyesha kughadhabishwa na yaliyomsibu mwenzao.
Jaribio na Bi Mbarire ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake
(Kewopa) kutaka kuzungumzia suala hilo lilizimwa na Spika Justin Muturi aliyesema kuwa hatua hiyo ni kinyume na Sheria za Bunge.

Kusifiwa
Hata hivyo, kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale aligusia suala hilo alipokuwa akishughulikia mswada mwingine, kwa kusema  Bi Gure kuitwa "msupuu" ni sawa na kusifiwa. Wabunge wanawake walilalama kwa sauti za juu, na kupelekea Duale ambaye ni Mbunge wa Garissa Mjini kuondoa kauli hiyo.